MAKAMBA MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA 48 WA JUIMUIYA YA WAISLAMU WAAHMADIYYA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu wa Waahmadiyya Tanzania utakafanyika kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Msongola, Manispaa ya Illala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo jijini humo na Katibu Mkuu Msaidizi wa jumuiya hiyo, Sheikh Abdulrahman Mohamed Ame katika Ukumbi wa Idara wa Habari Maelezo wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na mkuatano huo.
Amesema Waziri Makamba ataufungua mkutano huo wa siku tatu huku akibainisha jumuyiya hiyo imekuwa ikifanya mikutano miku kila mwaka lengo likiwa kukumbushana misingi sahihi ya dini Tukufu ya Islam, kukuza undugu na urafiki miongoini mwa wanajumuiya na wananchi kwa ujumla pamoja na kuhamasisha uwepo wa amani katika jamii.
" Jumuiya ya Ahmadiya ndio pekee miongoni mwa waislam iliyo na utaratibu wa Ukhalifa, ikiongozwa na kiongozi mmoja anayesimamia utendaji wa jumuiya katika kila nchi duninai kote hapa nchini jumuiya hii inao upekee wa kuwa j\umuiya ya mwanzo ya Kiislamu kutafsiuri Qurani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili mnamo mwaka 1953," amesema Sheikh Ame.
Amebainisha kuwa mkutano huo utajumuisha washiriki 4000 kutoka mikoa yote nchini na kuongeza jumuiya hiyo iko katika hatua za mwisho ukamilishaji wa uanzishwaji wa Kituo cha Redio kwa nia ya kusambaza mafundisho sahihi ya Islam na kushajisha uwepo wa amani katika jamii.
Amesisitiza kuwa kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni " Muslamu wa Kweli ni yule ambaye watu wengine wote wakaop salama dhidui ya shari ya ulimi wake na mikonoi yake'' akimaanisha kuwa Waislamu wana haja ya kuishi na kutenda kwa namna ambayo watu wengine watakuwa mashahidi kwamba Islam dini ya amani.
Aidha, amesema mkutano huo utahudhuriwa na baadhi ya washiriki kutoka nchi za nje zikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Uingereza huku akitilia mkazo viongozi wa kadhaa wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za dini na za kijamii wamealikwa.
Amefafanua kuwa jumuiya hiyo imekuwa ikitilia mkazo suala la amani kupitia Kiongozi Mkuu wa dunia, Hadhrat Mirza Masroor Ahmad ambaye amekuwa akitembelea nchi nyingi zikiwemo za Ulaya,, Amerika, Austaralia na Afrika kuzungumzia changamoto ya amani duni na jinsi ya kukabiliana nayo.
Pia amesema jumuiya hiyo iko mstari mbele katika kutoa huduma ya elimu kuanzia ngazi ya awali na Sekondari katika Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro na kubainisha kuwa kupitia asasi ya Humanity First wamewahi kutoa msaada wa vifaa tiba ikiwemo Mashine ya kupima Saratani ya Matiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), kugawa vitabu vya kujifunzia, kompyuta, vifaa vya maabara na madaftari pamoja na kusaidia Waathirika wa Janga la Tetemeko la Ardhi lilitokea mkoani Kagera.
Kwa upande wake, Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amewakarabisha waislamu na waamini wa madhehebu mengine kuhuhuria mkutano huo wenye lengo kuhamasisha kudumisha amani kwenye jamii.
No comments:
Post a Comment