Mange Kimambi, Wema Sepetu Watajwa Michango ya Lissu..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe amewashukuru Watanzania wanaoendelea kumchangia Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu akiwataja wanaoongoza katika kuhamasisha uchangiaji
mitandaoni akiwamo Mange Kimambi na Wema Sepetu.
Mbowe amesema mpaka leo Ijumaa jumla ya Sh204 milioni
zimepatikana katika michango hiyo pamoja na msaada wa hali ambao wamekuwa
wakipewa na Watanzania.
“Tunawashukuru wanaoendelea kuchangisha, tunamshukuru Mange
Kimambi kwa kuwahamasisha diaspora kuchangia na katika mitandao akishirikiana
na Wema Sepetu na wengine,” alisema Mbowe.
Mange alianzisha kampeni ya kumchangia
Lissu katika
mtandao wa Gofundme akilenga kupata dola za Marekani 50,000 na mpaka
kufikia leo saa 10.41 katika mtandao huo kiasi cha dola za Marekani 23,380
ilikuwa imepatikana ambayo ni wastani wa Sh51.3 milioni.
No comments:
Post a Comment