Manji yamkuta mengine, Maya Manispaa ya Temeke adai amepoteza sifa kuwa Diwani...Kwa Kushindwa Kuhudhuria vikao...#share
MEYA wa Manispaa ya Temeke,
Abdallah Chaurembo amesema mfanyabishara Yusuf Manji amepoteza sifa za kuwa
Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao vya kamati vya
halmashauri hiyo.
Amesema kwa kukosa vikao hivyo
Manji ambaye kwa sasa yupo katika gereza la Keko akikabiliwa na kesi
mbalimbali, amevunja kanuni za
Halmashauri pamoja na Sheria za Serikali za mitaa sura ya nane ya mwaka 1982.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meya Chaurembo alisema Manji amepoteza sifa kutokana
na kutoshiriki vikao hivyo huku akisisitiza mfanyabiashara huyo alimuandikia
barua Mkurugenzi wa manispaa hiyo Februari 20 mwaka huu ikitoa taarifa kutoweza
kuhudhuduria vikao kwa sababu za kiafya bila kuwasilisha uthibitisho wa
daktari.
''Vikao alivyokosa baada
ya kuandika barua yake ni vile vya tarehe 3 na 4 vya mwezi Machi, 18-19/5/2017
na 24-25/8/2017 hivyo sheria za
halmashauri za mwaka 2015 kifungu cha 72(c) ambacho kinatamka diwani pamoja na
majukumu mengine aliyonayo lazima ahudhurie mikutano ya halmashauri na kamati
ndogo ambayo yeye ni mjumbe bila kukaosa,'' amesema Chaurembo.
Amebainisha kuwa
Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Nassib Mmbagga alimwandikia barua mafanyabiashara
huyo ikimtaka kuwasilisha taarifa za kidaktari kuthibitisha matatizo ya kiafya
kama alivyoeleza kwenye barua yake lakini hakutekeleza huku akionekana kwenye
vyombo vya habari akiendelea na shughuli zake.
Amesisitiza kuwa Manji
aliandika barua Mei 22 mwaka huu kwa mkurugenzi ikieleza kutoweza kuhudhuria
vikao hivyo kwa sababu za kiafya bila kuweka wazi uthibitisho wowote wa daktari
na kwamba aliweka wazi nia yake ya kutaka kujiuzulu kama hali yake ya afya
haitaimarika.
Ameongeza kuwa sheria za
serikali hizo sura hiyo ya mwaka huo kifungu cha 25 (5) kinaeleza kuwa mjumbe
wa Baraza la Madiwani ambaye hakuhudhuria vikao vtatu mfulilizo bila taarifa
yoyote ya maandishi anajiondoa katika nafasi yake na kwamba kanuni za kudumu za
manispaa za mwaka 2015 zinaeleza wazi kiti hicho kitakuwa wazi endapo mjumbe
bila sababu ya kuridhisha au kibali cha maandishi cha mwenyekiti atakosa
kuhudhuria mikutano mitatu nafasi yake inatakiwa kuwa wazi (kifungu cha 73 (1)
(m).
Amefafanua kuwa Manji
hakuhudhuria vikao vya mikutano ya halmashauri iliyofuatana bila kutoa taarifa
ikiwemo ya Februari 3 mwaka huu, Machi 24, 2016, Juni Mosi mwaka jana, Aggosti 25, 2016, Novemba 24,2016 na Februari
14 na 15 mwaka huu.
Aidha, amesema vikao vya kamati ambayo yeye alikuwa mjumbe
hakuhudhuria vya tarehe 18/3/2016, 17/8/2016,
8/11/2016 na 2/2/2017 huku akibainisha hata mikutano aliyotoa taarifa alishindwa kuthiubitisha taarifa za ugonjwa.
Pia amesema tayari ameshamwandikia barua Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene kumjulisha uvunjivu wa kanuni
za kiutendaji uliofanywa na Manji hivyo waziri mwenye mamlaka ya kutangaza
nafasi hiyo iko wazi.
Na Hussein Ndubikile



No comments:
Post a Comment