Ona jinsi TECNO inavyoendelea kutoa burudani ya SPARK kwa watanzania katika mitaa mbalimbali nchini...Kilele chake kuwa jijini Mwanza kwa washindi kuta.....#share

                       
                            SHINDA TECNO SPARK MTAANI KWAKO. 
                
KAMPUNI ya simu ya TECNO imekuja kivingine kwa kuwaletea wateja wake  na wanatanzania kwa ujumla  burudani ya SPARK katika mitaa mbalimbali ya majiji yanayopatikana nchini Tanzania.



Mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na Tanga imekua ya kwanza kushuhudia  michezo mbali mbali ya kuvutia inayoletwa na TECNO katika mitaa mbalimbali ya mikoa hiyo ikiwa na madhumuni makubwa ya kuwapa burudani wateja wao na kuitambulisha simu mpya kabisa ya TECNO SPARK.

Watoa burudani hao wa TECNO wanapita katika mitaa mbalimbali ikiwemo kihonda, kichangani, msamvu katika mkoa wa morogoro huku maeneo kama mabanda ya papa, magomeni, muheza, pongwe na korogwe mkoani Tanga yakiwa katika mtiririko  wa kutembelewa na burudani hizo kabambe kutokea TECNO.



TECNO inawapa nafasi wanatanzania wote popote walipo wanachotakiwa kufanya endapo wataliona basi la kampuni ya TECNO likiwa limeandikwa TECNO SPARK, wajiunge popote pale ambako burudani zitakua zinatolewa katika mitaa yao hivyo wataweza kujishindia zawadi za aina mbalimbali  ikiwemo simu mpya kabisa ya TECNO SPARK..

TECNO SPARK  ni moja kati ya matolewa bora mapya ya simu kutokea TECNO yanayofanya vizur sokoni kwa kupendwa watanzania wengi kutokana na sifa zake kwani ina kamera nzuri  ya 13mp nyuma , pia ina teknolojia ya usalama wa vidole huku umbo lake likiwa ni kuvutio kikubwa katika macho pale ambako mtumiaji anakua ameishika mkononi. Kioo chake ni 5.5 inchi, 16 gb za kuweka vitu ndani pamoja na 2 gb ram.
 

Burudani hizi za TECNO zitakua na kilele chake katika ukumbi wa burudani wa club Rock bottom mkoani Mwanza, ambapo wapenzi kampuni ya TECNO Mobile watatangazwa walioweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu mpya ya   SPARK.

Bado  hujachelewa mkoani Morogoro, Tanga, Arusha, Manyara pamoja Mwanza unaweza kupiga picha endapo utalion basi la TECNO SPARK au burudani katika mtaa  wako alafu weka katika mitandao yako ya kijamii aidha Facebook, twitter au Instagram ukiandika #vimbanaspark ili uweze kujishindia zawadi kemkem kutokea TECNO.
 



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search