Mbunge CCM atoa ufafanuzi sababu ya kukodi ndege ya Lissu kwenda matibabu Nairobi, Kenya...#share

MBUNGE wa Mpendae kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Salim Hassan Turky amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumemlipa fedha alizowadhamini ili kufanikisha ukodishwaji wa ndege iliyomsafirisha  Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Tundu Lissu kwenda jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu baada ya kupigwa risasa akitokea Mkoani Dododoma.


Ametoa ufafanuzi huo leo kutokana na Kauli iliyotolewa na Spika wa Bunge Job Ndugai kwamba Turky ndiye aliye gharamia fedha za ndege jambo ambalo lilipingwa na chadema na kudai kuwa anapotosha umma.

Aidha Turky amesema kuwa aliamua kufadhili fedha hizo kutokana na kwamba hawakuwa na fedha taslimu za kuweza kulipia ndege.

“Tusifanye tukio la Tundu Lissu kuwa la siasa. Mimi binafsi tukio zima la mbunge mwenzangu limenisikitisha sana limenisononesha sana. Nikiwa kama kamishna wa Bunge lakini pia ni binadamu kuna kuzaliwa na kufa,”amesema.

“Kwa hiyo tukio hilo lilipotokea tuliitwa na makamishna wote na Spika wetu wakiwemo Mbowe (Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani) Msigwa na timu yake. Kwanza ndege ilikuwepo pale Airport ambayo ilikuwa imeshaagizwa na Bunge iko stand by kumpeleka moja kwa moja Muhimbili.”

Amesema walichoamua ni kuwa aende moja kwa moja Nairobi nchini Kenya lakini ndege hiyo haikuwa na kibali cha kwenda nchini humo na kwamba ili uweze kwenda nchini humo unalazimika kuwa na marubani wawili.

Hata hivyo, amesema Spika Ndugai alihangaika kupata kibali cha ndege iliyokuwepo uwanjani ili iweze kumpeleka mgonjwa Nairobi.

“Wakati mambo yote tayari rubani wa ndege akasema kuna kitu kinaitwa landing Instrument ambayo ile ndege haina kwa hiyo haitaweza kuruka,” amesema.

Amesema kutokana na majibu hayo waliingiwa na sitofahamu watafanya nini lakini yeye aliingia katika uzoefu wake aliopewa na Mungu kwa kutafuta ndege kwa ndugu zake ambao wanafanya nao biashara sana.

“Nikawaambia ndege ipo wakatoa nauli zao za ghali ghali kwa sababu tunajuana wakakubali kutusaidia kwa dola 9,200 pamoja na ambulance (gari la wagonjwa) mimi ndio niliyoita kwa kubaliana na Mbowe na Msigwa kwamba Turky haya mambo yasimamie baadaye…na ndicho kilichofanyika,” amesema.

Aidha Turky ameendelea kueleza kuwa walipofika nchini Kenya siku ya pili walipaswa kuwa ametoa fedha hizo lakini haikuwa hivyo mpaka leo Septemba 14, 2017 majira ya saa sita mchana alipowasiliana na wahusika aliambiwa kuwa CHADEMA walikuwa wameshalipa hizo fedha.

 Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search