News Updates: Hii hapa taarifa njema kutoka Nairobi, Kenya maendeleo ya Rais wa TLS, Mbunge Tundu Lissu...#shaare

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesem Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu ameanza kuongea na kula.


Hayo yamebainishwa leo jijini Nairobi nchini Kenye Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari, amekanusha taarifa zinazoenea kuwa Lissu amepata maambukizi ambayo yanatishia maisha yake.

“Hali ya Lissu inabadilika kila siku, ni wahakikishie tu wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake,” amesema Mbowe.

Aidha mbowe ameeleza kwamba Mbunge huyo wa Singida Mashariki ameweza kuonana na baadhi ya watu waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.

"Pamoja na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search