Mbunge Kubenea Aendelea Kusota na Polisi...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesafirishwa leo alfajiri kwenda
mjini akitokea jijini Dar es Salaam, anaandika
Mwandishi wetu.
Kubenea amefikishwa mjini Dodoma baada ya jana kukamatwa
akiwa hospitali jijini Dar es Salaam alipoenda kupata matibabu na kulazwa
kituo cha Polisi cha Oysterbay kabla ya leo alfajiri kupandishwa ndege kwenda
kutoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge.
Mbunge
huyo amekamatwa kwa amri ya Spika Job Ndugai ambaye wiki iliyopita aliviagiza
vyombo vya dola kumsaka popote alipo Mbunge huyo na kumkamata.
Kosa la kukamatwa Kubenea lilitokana na kutofautina na Spika
kuhusu idadi halisi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu mjini Dodoma .
Mbunge huyo alisema Lissu alipigwa risasi 38, huku Spika
akisema idadi ilikuwa 32 na baada ya kupishana huko, aliagiza Kubenea
akamatwe ili akatoe ushahidi kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge ambayo
pia inaendelea kuchunguza tukio hilo.
Miongoni waliowahi kusafirishwa kwa ndege ni pamoja na Ester
Bulaya ambaye ni Mbunge wa Bunda (Chadema), kwa amri ya Spika
pamoja na Freeman Mbowe aliyesafirishwa kwa ndege pia kwenda jijini Arusha
kuhudhuria kwenye kesi.
Taarifa zinasema Kubenea amewasili leo mjini Dodoma saa moja
asubuhi na kwamba badio afya yake siyo nzuri na hivyo hajui kama anaweza
kusimama na kuhojiwa na kamati hiyo.
Aidha, taarifa hiyo imesema Kubenea bado ana maumivu makali
sana na kwamba hajaambiwa atahojiwa wapi na saa ngapi.
Kubenea amemshukuru Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Mandeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye amesema amesaidia katika hali yake
ya ugonjwa mpaka kufika Dodoma baada ya kukutana naye kwenye ndege leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment