Mchungaji Mashimo Amtabiria Uhuru Kenyatta Kushinda Kiti cha Urais Kwa Mara Nyingine ....Habari Kamili Hii hapa na Matukio360....share..#
MCHUNGAJI wa Mitume na Maaskofu Tanzania David Mashimo (Komando
Mashimo) amesema kuwa mgombea nafasi ya urais kupitia Mungano wa NASA Nchini
Kenya Raila Odinga hawezi kuwa rais wa Taifa hilo kutokana maono aliyonyeshwa
na Mungu.
Mchungaji huyo wa kanisa la True Gospel Seven day Church
amesema hayo wakati wa mkutano wake na wanahabari uliuofanyika jijini Dar es
salaam.
Amesema kuwa tangu novemba 26 mwaka Jana Mungu amemuonyesha
maono kuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru kinyatta ataendelea
kuwa rais wa Kenya licha ya mahakama ya Juu ya nchi hiyo kuzuia ushindi wa
Kinyatta baada ya Odinga kushindwa kukubaliana na matokeo yaliyompa ushindi.
Komando mashimo amesema kuwa Odinga hana mpango mzuri
na nchi ya Kenya bali anatumiwa na makundi ya watu kwa maslahi binafsi.
Amesema kuwa jaji mkuu wa mahakama kuu ya Kenya Jaji Malaga
ametoa hukumu hiyo kwa shinikizo la watu ambao hawaitakii mema nchi ya Kenya
lakini akasisitiza kuwa Uhuru Kinyata atashinda kwa Mara
nyingine katika uchaguzi wa marudio kama ilivyotangazwa na tume ya
uchaguzi ya nchi hiyo.
Pia amewaomba viongozi wa kiroho kuacha kuchanganya mambo ya
dini na masuala ya kisiasa.
Komando mashimo amefanya tukio la kumpaka mafuta na
kumwapisha Mwinjiristi na Mwimbaji wa Nyimbo za Dini Amon Mwakalukwa kama
ishara ya kiimani ya ushindi wa Uhuru Kinyatta.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment