Simba Yashindwa Kufurukuta Mbele ya Mbao Fc...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
Klabu ya Simba imeshindwa kufurukuta mbele ya Mbao Fc ya Jijini Mwanza baada ya kutoka sare ya 2-2.

Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba Simba ndiyo ilikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza ambapo hadi kipindi cha kwanza kinaisha timu hiyo ilikuwa ikiongoza kwa goli hilo.
M
namo kipindi cha pili Mbao walianza kwa kasi na hatimaye kupata goli la kusawazisha lakini hazikupita hata dakika mbili Simba waliongeza goli lapili.
Wakati Mchezo ukiwa unaelekea mwishoni vijana dwa Mbao wameweza kuchomoa na mchezo kumalizika kwa sare hiyo.
Hiyo inakuwa ni sare ya pili kwa Simba kwa musimu huu wa ligi kuu ya VPL wakati kwa Mbao nsiyo kwa mara ya kwanza wanapata pointi.
Magoli ya Mbao FC yamewekwa kimiani na Kiyombo dakika ya 47 na Maganga dakika ya 81 huku yale ya Simba SC yakifungwa na Kichuya dakika ya 16 na Kotei dakika ya 49.
No comments:
Post a Comment