Merkani na China kuijadili Korea Kaskazini..Soma Habari Kamili na Matukio360..#shaare

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson na mwenzake wa China Wang Yi
Image captionWaziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson na mwenzake wa China Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson yuko mjini Beijing kufanya mazungumzo na viongozi wa China.
Ajenda kuu katika mkutano huo ni mzozo kati ya Korea na Marekani.
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni
Utawala wa Trump unaamini China ina umuhimu mkubwa, katika juhudi za kuishurutisha Korea Kaskazini kusitisha uundaji wa silaha zake za Nuklia.
China imeonyesha kujitolea kwake katika utekelezaji wa vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi ya taifa hilo.
Siku ya Alhamisi, Beijing ilitangaza kuwa mashirika ya Korea Kaskazini yanayoshirikiana na China hayana budi kufungwa.
Ziara ya Tillerson inakuja huku Rais Trump akitarajiwa kutembelea taifa hilo baadaye mwezi Novemba.
BBC

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search