Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa wanyama pori (TAWA) Dkt. James Wakibara anaendelea na ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya TAWA na amewataka watumishi wafanye kazi Kwa kujituma bila kulazimishwa, na kuepuka vitendo vya rushwa, na kuwataka kuzingatia Tunu za TAWA (Core Values) ambazo ni uwajibikaji, Uadilifu, Ubunifu, kushirikiana na wadau, na kuheshimu uhifadhi. Aidha, DKt. Wakibara amewataka watumishi watatue matatizo yao kwa kufanya vikao vya menejimenti mara kwa mara
Dkt. Wakibara amesema TAWA ni Mamlaka mpya iliyoanzishwa kwa lengo la kuleta ufanisi, tija, kuboresha maslahi ya watumishi, na kuendeleza uhifadhi wa Raslimali za wanyamapori wote walioko nje ya hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kutokana na hali hiyo amesisitiza watumishi watambue wajibu wao na wabadilike kiutendaji na kukuza mawasiliano mazuri na wadau mbalimbali wa uhifadhi.
Mwisho amewaeleza watumishi kuwa TAWA bado inashughulikia muundo wake, sheria za TAWA, na kukamilisha makabidhiano machache yaliyobaki kati yake na Idara ya Wanyamapori. Taarifa hii imetolewa na Bw. Twaha Twaibu-Afisa Habari na Mahusiano wa TAWA
|
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Dkt. James Wakibara (wanne kutoka kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa pori la Akiba Rukwa/Lwafi |
|
Dkt.Wakibara (katikati) akisikiliza kero za watumishi |
|
Kaimu mkurugenzi wa ulinzi wanyamapori Bw. Mabula Misungwi akizungumza na watumishi |
|
Dkt. Akisikiliza watumishi hawaonekani kwenye picha hii. |
No comments:
Post a Comment