Mej. Generali mstaafu Khamis Semfuko (M/kiti wa Bodi-TAWA) akipokea salamu ya heshima kutoka kwa wahitimu Maafisa wanyamapori 59 kutoka vituo mbalimbali vya TAWA baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi huko katika kambi ya Mlele, Mkoani Katavi tarehe 30/9/2017.
|
Pichani juu👆 na chini 👇askari wakitoa heshima Kwanzaa mgeni rasmi Men. General Semfuko |
Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania-TAWA inaendesha mafunzo kwa watumishi wake kwa kushirikiana na hifadhi za Taifa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuwaanda kuingia katika mfumo wa jeshi usu (Paramilitary) kutoka mfumo wa kiraia. TAWA haya ni mafunzo ya awamu ya nne tangu yaanze, watumishi zaidi 260 wameshahudhuria. Mahafali ya leo tarehe 30/9/2017 yamehusisha maafisa wanyamapori 59. Mgeni rasmi alikuwa Mej. General (Mstaafu) Khamis Semfuko akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Dkt. James Wakibara.
Aidha kulikuwa na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Mgeni rasmi alikemea vitendo vya ujangili na kuomba wahitimu watumie ujuzi wao kukabiliana na ujangili wa raslimari za wanyamapori.
Aliongeza kwa kuwaomba wakuze ushirikiano na wananchi wanaoishi kandokando na hifadhi.
Mkurugenzi Mkuu wa TAWA aliwaeleza wahitimu watambue kuwa TAWA bado ni changa hivyo inabidi wafanye kazi kwa kuzingatia TUNU za TAWA ambazo ni uadilifu, ubunifu, ushirikiano na wadau, uwajibikaji na kufanya kazi kufuata misingi ya uhifadhi.
|
Mgeni rasmi(wa pili kutoka kushoto) kwenye picha ya pamoja na wahitimu
|
|
Mahafali hayo yalihudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Dr. James Wakibara |
|
Dkt. Wakibara mwenye kofia nyekundu akipokea heshima toka kwa maafisa wanyamapori |
|
Mgeni rasmi akishuhudia ulengaji wa shabaha |
|
Askari wakionyesha umahiri katika zoezi la ulengaji shabaha mbele ya mgeni rasmi
|
|
Bw. Mabula Misungwi(kaimu mkurugenzi wa ulinzi raslimari za wanyamapori) alikuwepo |
|
Picha ya walimu (wenye T- Shirt nyekundu) na mgeni rasmi |
|
Mgeni akmpongeza kiongozi wa gwaride baada ya kumtunuku cheti |
Picha na habari na Afisa Habari na Mahusiano - TAWA.
No comments:
Post a Comment