Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aziagiza Serikali za Mitaa na Ngazi Nyingine Mkoani Pwani Kuimarisha Ulinzi Maeneo ya Viwanda na Wawekezaji....Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka serikali za vijiji na
ngazi nyingine mkoani Pwani, kujikita kuimarisha ulinzi katika maeneo
mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kulinda mali na usalama wa wawekezaji na
watanzania kijumla.

Amesema haijajulikana hadi sasa nia na dhamira ya watu
wasiojulikana wanaojihusisha kupoteza maisha ya watu ,na ni hatari endapo
watajiingiza katika maeneo ya uwekezaji kwani hakuna mwenye uhakika wa azma
yao.
Aidha Majaliwa ,ametoa wiki mbili kwa waziri wa maji
kutathmini matokeo ya mwenendo wa mradi wa maji wa WAMI ,ili kutoa utaratibu na
kama sheria inaruhusu kuvunja mkataba ikiwa mkandarasi ameshafikia kiwango cha
asimilia 50 ya utekelezaji.
Waziri huyo ,pia ameziagiza halmashauri nchini kuona umuhimu
wa kutenga fedha kwa ajili ya kununua magari ya zimamoto yatakayosaidia
kudhibiti majanga ya moto yanapotokea hususan kwenye maeneo ya uzalishaji na
viwanda.
Katika hatua nyingine amelitaka shirika la umeme
Tanesco,Dawasco kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya umeme na maji katika
maeneo yenye uwekezaji ili kuvutia wawekezaji.
Alitoa rai hiyo,wakati wa ziara yake ya siku moja
,aliyoifanya mkoani Pwani kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KEDS
kilichopo Kibaha,na cha kutengeneza vigae Twyford Ceramics Ltd/Pingo,Chalinze
,Bagamoyo.
Majaliwa ,alieleza kuwa ni lazima raia mmoja mmoja na jukumu
la kila mmoja kusimamia kulinda nchi kuanzia maeneo wanayoishi .
Alisema serikali imejipanga kuendelea kusimamia amani na
utulivu,ambapo amewataka wananchi waiunge mkono serikali kupambana na wahalifu
wasio na nia njema na serikali.
“Hatuna uhakika kwa watu hawa wanaofanya vitendo vya
ovyo,watanzan ia waungane na serikali,kupambana ili wasije kuingia kwa
wawekezaji na kupoteza ndoto za serikali za kupata wawekezaji “alisema
Majaliwa.
Akizungumzia tatizo la uhaba wa maji ,alisema mradi wa WAMI
ulikuwa ukamilike tangu mwezi July mwaka huu.
Alisema alitembelea mradi huo mwezi juni mwaka huu ukiwa
chini ya asilimia 38 na kusema mkandarasi akiendelea kusuasua watamfukuza na
kutoa agizo ikifika mwezi huu wafikie asimilia 80.
“Nilitaka kuja mwezi huu lakini nikaambiwa speed ni ndogo na
bado hali hairidhishi,na mkandarasi hajamaliza”mbunge wa Chalinze Ridhiwani
Kikwete amekuwa akiuliza juu ya kukwama kwa mradi huo” ;”Nimetoa wiki
mbili kwa waziri aangalie dhamana ya kampuni kwenye ubalozi wao wa India na
kuangalia sheria namna ya kufanya ama kukamilisha mradi kwa muda mfupi
uliobaki”alifafanua.
Kuhusu nishati ya umeme Majaliwa,alisema serikali ipo mbioni
kutekeleza mradi mkubwa wa umeme stiegler’s gorge katika chanzo cha mto Rufiji,
utakaozalisha megawatts 2,100 zitakazoondoa kama si kumaliza upungufu wa umeme
uliopo.
Aliitaka halmashauri ya Chalinze,ijipange kwa matumizi bora
ya ardhi ili kuondoa migogoro na kuondoa usumbufu kwa wawekezaji.
Kuhusu suala la zimamoto ,Majaliwa alisema mkoa huo kwasasa
una viwanda vikubwa hivyo wakati serikali ikipokea changamoto ya uhaba wa vifaa
na magari ya zimamoto ,halmashauri ijipange kupitia bajeti zao.
“Viwanda hivi ni vikubwa vinajengwa ,kiwanda hiki cha KEDS
kina jengo hilo hapo lenye urefu wa mita 30 juu,tuombe mungu moto usitokee
,unawezaje kuzima moto kwa maji ya kwenye ndoo ,ipo haja ya kuangalia namna ya
kutatua changamoto hii”
“Dar es salaam ambako ni mji wa kibiashara serikali itasaidia
katika kununua mitambo ya kusaidia kuzima moto kutegemea ukubwa wa majengo
yaliyopo”aliongeza Majaliwa.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara,alitoa rai kwa
halmashauri ya Mji wa Kibaha kuboresha barabara zilizopita mitaani na
kuhakikisha mitaa yote iwe na barabara bora kwa kufumua zisizofaa na kuchonga
barabara zenye viwango.
Pamoja na hayo ,Majaliwa alibainisha uwekezaji kama huu
unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda
ambapo itaongeza pato la nchi na itazalisha ajira kwa wingi
No comments:
Post a Comment