Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Kibanda Asema Uhuru wa Habari Nchini Unabanwa..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share



MWENYEKITI wa jukwaa la wahariri Tanzania Absalom Kibanda amesema kuwa upatikanaji wa taarifa unabanwa na sheria nyingi hapa nchini ambazo zinanyima uhuru wa kupata taarifa.



Aidha kutokana na sheria hizi huwa zinakuja na kauli za vitisho ambazo zinatumiwa na wasimamizi vibaya huku wamiliki wa vyombo vya habari wakitishwa kwa kaulili mbalimba na kupelekea kupoteza lengo la upatikanaji wa habari.

 Waandishi wanakuwa na wakati mgumu wa uwasilishaji wa taarifa kwani wanatoa ama kuandika taarifa kwa uwoga kutokana na vitisho hivyo kupelekea taarifa kuwa finyu, kutokana na kuogopa kauli za vitisho kutoka kwa wasimamizi wa sheria hizoAmesama hayo leo katika kongamano liliofanyika jijini Dar es salaam la kujadili siku ya upatinaji wa taarifa na kusema kuwa Tanzania kuna sheria nyingi ambazo zinatungwa kwa lengo la kuminya upatikaniwa taarifa ikiwemo sheria ya mtandao, sheria usalama wa taifa, sheria hudama za habari, na sheria za takwimu  hivyo sheria hizi zimetungwa mahususi kwa lengo la kuminya wanahari na vyombo vya habari.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search