Taarifa za Tundu Lissu Zamponza Mfanyabiashara Mwakihaba..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


MFANYABIASHARA Mbutusyo Mwakihaba (40) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo kwamba amemuona Kachero karibu na Hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Image result for hali ya tundu lissu mbaya
Mshtakiwa huyo alisomewa kosa lake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa na Wakili wa Serikali, Janeth Magoho.

Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa September 11, 2017 huko Dar es Salaam kupitia mfumo wa kompyuta alisambaza taarifa hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kusema “Huyo ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose ameonekana Nairobi karibu na Hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu mwacheni mwenzenu.”

Wakili huyo wa Serikali, Magoho alidai kuwa mshtakiwa aliyatoa maneno hayo kwa nia ya kupotosha umma ambapo baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja anatakiwa kusaini bondi ya Tsh Milioni 5 ambapo kesi imeahirishwa hadi October 12, 2017 kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa ameshindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kupelekwa rumande.
Chanzo: Millard Ayo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search