PM Awatumia Salamu Watu Wasiojulikana....Asema Serikali Haita....#share
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali haitafumbia macho matukio ya mashambulizi wanayofanyiwa watu mbalimbali wakiwepo viongozi na kuwataka wabunge na wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati jeshi la polisi likiendelea kufanya uchunguzi.
Waziri Majaliwa amesema hayo wakati akiahirisha vikao vya
mkutano wa nane wa bunge la 11, na kusema vyombo vya dola vinaendelea kufanya
uchunguzi ili kuwabaini watu wasiojulikana wanaojihusisha na vitendo
hivyo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
"Serikali haitofumbia macho matukio ya kihalifu
yanayotokea nchini, vyombo vya dola tayari vimeshaagizwa kuhakikisha
wanawatafuta wanaohusika na vitendo vya kihalifu na kukamatwa ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yao", amesema Waziri Majaliwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Adad Rajabu ameliomba bunge kuongeza muda
ili kuweza kukamilisha kazi ya kufanya uchunguzi wa matukio ya kujeruhiwa,
kuvamiwa pamoja na kufuatiliwa kwa baadhi ya wabunge ili kuweza kukamilisha
kazi hiyo.
Aidha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amehairisha vikao vya
bunge leo hadi Septemba 7 mwaka huu ambapo litafunguliwa tena.
No comments:
Post a Comment