Rais wa Zamani TFF Malinzi, Wenzake Kuendelea Kusota Rumande...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzanai (TFF) Jamal
Malinzi na wenzake wanaendelea kusota rumande baada ya kesi yao kuahirishwa
kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika.

Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya
utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza
Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika,
hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo
hadi October 5, 2017.
Mbali ya Malinzi, washitakiwa wengine ni aliyekuwa Katibu
Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga
ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni
Dola za Marekani, 375,418.
Na Mwandishi Wetu.
No comments:
Post a Comment