Wakati Jumamosi Hii Timu za Borussia Monchengladbach na Borussia Dortmund zikikutana...Mdau wa Michezo Matukio360 Imekusogezea Hapa Rekodi Moja ya Bundelsliga Inayoziunganisha...#share
Kuna rekodi moja ya Bundesliga inayoziunganisha Borussia zote
yaani Monchengladbach na Dortmund.

Wakiwa wanajiandaa kukutana katika dimba la Signal Iduna Park
katika mechi kali ya wiki hii Siku ya jumamosi, kitu cha uhakika ni kwamba
rekodi hiyo haitavunjwa.
Kwenye mechi ya mwisho wa msimu wa 1977/8, Monchengladbach
waliingia uwanjani wakiwa na idadi sawa ya point na Cologne, lakini wakiwa
nyuma kwa tofauti ya magoli 10 nyuma ya wapinzani wao ambao walikuwa
wanatazamia kushinda kirahisi mchezo wao dhidi ya St Pauli.
Kwenye mchezo uliolalia upande mmoja zaidi katika historia ya
Bundesliga, Monchengladbach walifunga mabao sita katika kila dakika 45 za mchezo
bila majibu hivyo kupelekea matokeo ya 12-0 baada ya kipenga cha mwisho kulia.
Ikiwa ni rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa ndani ya Bundesliga.
Tangu kipindi hicho Monchengladbach hawajakaribia hata kidogo
kushinda ubingwa wao wa sita huku wapinzani wao wakishinda Ubingwa huo mara
tano na kuwa ndio hasimu mkubwa wa Bayern Munich.
Mfungaji bora wa msimu uliopita Pierre Emerick Aubameyang
ameendelea kutikisa nyavu bila wasi, huku Monchengladbach wakiwa na vijana
machachari Lars Stindl na Thorgan Hazard, ambao wanachezea timu za taifa,
Ujerumani na Ubelgiji.
Mchezo huu pia utakuwa ni kwanza kwa kiungo Mahmoud Dahoud
kukutana na timu yake ya zamani tangu alipojiunga na Dortmund majira ya joto.
Nafasi yake katika kikosi cha Monchengladbach imejazwa na kinda kutoka Uswizi Denis
Zakaria ambaye amepata sifa kedekede kutoka kwa kocha wake.
“Ni burudani unapomtazama Denis namna alivyozoea. Hakika
ameshatulia ndani ya Bundesliga”, Kocha wa Monchengladbach Dieter Hecking
alisema, “Lakini sasa anahitaji kuendelea kucheza vizuri bila kuonyeshwa kadi”,
aliongeza.
Watazamaji kote nchini wataweza kutazama mchezo huu MUBASHARA
kupitia Chaneli ya World Football Saa 1:30 Usiku Jumamosi hii.
Hii ni moja kati ya mechi zinazofanya Bundesliga iwe na mvuto
wa kipekee na pia nafasi kwa waafrika kumtazama muafrika mwenzetu Aubameyang ambaye
ni kinara ndani ya timu ya Dortmund.
Na Mwandishi Wetu.
No comments:
Post a Comment