Breaking News: Serikali Iko Tayari Kugharamia Matibabu ya Lissu...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share

SERIKALI imesema ipo tayari kugharamia matibabu ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu ambaye kwa sasa hivi yupo Jijini Nairobi kwa matibabu kufuatiwa shambulio alilolipata Septemba 7,mwaka huu Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa Jijini Tanga na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Waziri Ummy Mwalimu alisisitiza Serikali inasubiri kupata maombi kutoka kwa familia ya mgonjwa ikiambatana na taarifa rasmi kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa”Serikali ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mhe.Lissu popote Duniani”. Akiwa kama Mtanzania na Mbunge,Serikali inayo wajibu wa kugharamia matibabu yake hadi apone ili aweze kuendelea na kazi ya kuwahudumia Watanzania na wana Singida Mashariki.
itakayotolewa na Mhe.Lissu au Mwanafamilia wa karibu kama taratibu za Kidaktari zinavyoelekeza.

Aidha, Serikali imeshangazwa na dhana ya kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutokea matapeli watakaochangisha Watanzania fedha kwa madai kwamba Mbunge huyo amekosa hela za matibabu.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto anawashukuru Madaktari wa watoa huduma wote wa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kuokoa maisha ya Mhe.Lissu na kumtakia apate nafuu haraka

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
21/9/2017

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search