Spika Ndugai Atoboa Siri ya Ugonvi Wake Dhidi ya Wabunge Zitto, Kubenea na Lema... #share

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai kwa mara nyingine amezungumzia sakata lake dhidi ya Wabunge Zitto Kabwe , Sued Kubebea na Godbless Lema na kusema kuwa yeye hana tatizo na lolote dhidi yao.

Lakini Ndugui amedai kuwa yeye ni binadamu hivyo mtu anapomnyanyasa na kumdhalilisha hutumia mamlaka aliyonayo kufanya Uaamuzi.

Ndugai amesema kuwa yeye kama kiongozi wa Bunge anamamlaka na madaraka makubwa kuliko hata yaliyoandikwa na kusisitiza kuwa anao uwezo wa kumsimamisha Mbunge asiongee chochote bungeni mbaka muda wa mbunge huyo utakapokwisha.

"Siyo kila kitu huandikwa katika mahusiano ya kikazi lakini kiongozi wako wa kazi ana mamlaka na madaraka makubwa kuliko hata yaliyoandikwa si kila jambo lazima liwe ni kanuni, narudi tena nimesikia watu wakibisha bisha ninao uwezo kama spika, zipo kanuni zinamruhusu Spika wa Bunge kwa kadri anavyoona inafaa kwa busara yake namna gani aongoze bunge, huwezi kuwa unatukana bunge unamtukana huyo spika halafu huyo huyo Spika anakupa nafasi uzungumze kwa sababu yeye ni malaika? Mimi ni binadamu mwenye damu na nyama kama wengine" amesema Ndugai.

Aidha ameendelea kusema kwamba Bunge aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kupotosha umma au kumzungumza mambo ya bunge kwa njia isiyo na staa kupitia mitandao hiyo ya kijamii na kumdhalilisha yeye na kusema yeye pia atatumia mamlaka yake kuona anafanya nini juu ya wabunge hao.

"Kwa jinsi unavyoninyanyasa na kunidhalilisha mbele ya watu na mimi nitatumia madaraka yangu na mamlaka niliyonayo niliyopewa na nchi na Mungu kuona nini nifanye katika mamlaka niliyonayo" amesitiza Ndugai.

Ndugai amesema kuwa ana uwezo wa kumzuia mbunge Zitto Kabwe asizungumze chochote ndani ya bunge kwa kipindi chote cha ubunge

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search