sPORTS nEWS: Je Simba kama Yanga Nayo kuvutwa Shati na Matajiri wa Madini Mwadui?... Ni leo baada ya dakika 90..#share
KLABU ya Simba SC ambayo inatajwa kuwa na kikosi cha gharama Zaidi
leo inajitupa uwanjani katika mchezo wa raundi ya tatu katika mchezo wa Ligi
Kuu Soka Vodacom Tanzania Bara kukabiliana na Matajiri wa Madini ya Almasi kutoka
mkoani Shinyanga Mwadui FC.

Mchezo huu utapigwa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam majira ya saa 10.00 jioni. Itakumbukwa mechi ya kwanza Simba ilishinda
goli 7-0 dhidi ya kikosi cha Ruvu Shooting na kasha kutoka suluhu baina yake na
Azam FC.
Wakati matokeo ya Simba katika mechi mbili za awali yakiwa
hivyo kwa upande wa Mwadui FC kwenye
mechi mbili za awali wameshinda moja na kupoteza moja.
Itakumbukwa jana klabu ya Yanga ilivutwa shati na klabu ya
Maji maji ya Songea kwa kulazimishwa sale ya goli 1-1. Hivyo Simba itaingia ikihitaji kuwa furahisha mashabiki
wake ili kuwazodoa mashabiki wa Yanga.
Je nani atakuwa ibuka mshindi katika mtanange huo. Je Okwi
ataibebe Simba? Tusubiri tuone baada ya dakika 90.
No comments:
Post a Comment