sPORTS nEWS: Azam yachekelea kucheza Chamazi na Simba, Yanga...#share
TIMU ya Azam FC imefurahia uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuwaruhusu kuutumia uwanja wao wa Azam Complex uliopo
Chamazi kwa mechi zake zote za nyumbani za Ligi Kuu Tanzania ikiwemo dhidi ya
Yanga na Simba .
Kwa mara ya kwanza vigogo vya soka nchini, Yanga na Simba
zitacheza katika uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na Azam FC, iliyoanzishwa
mwaka 2007.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Azam FC, Philipo
Alando alisema wamefurahia kupata fursa ya kuutumia uwanja wao wa nyumbani kitu
walichokuwa wanakililia.
“Ni jambo jema, tunafurahi kuona TFF hii inatoa makandokando
yote ambayo yalikuwa magumu kufanyika huko awali, kama kuruhusu uwanja huu wa
Chamazi kutumika kwa michezo yote.
Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba ndio watakuwa wa kwanza
kuandika historia ya kucheza na Azam FC kwenye uwanja huo katika mchezo wa Ligi
Kuu ta Vodacom, Jumamosi hii.
Kwa upande wa mabingwa watetezi ligi hiyo, Yanga itashuka
Chamazi Complex kuwavaa Azam katika mchezo wa mwisho wa kufunga mzunguko wa kwanza
wa ligi hiyo, Desemba 29 mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kikosi kazi, kilichopewa kazi
maalumu ya kupitia upya ratiba iliyokuwa imeandaliwa awali kuifanyia
marekebisho, kumaliza majukumu kazi yake juzi na kutoa ratiba mpya inayoonesha
uwanja huo kuanza kutumika kwa michezo mikubwa na miamba hiyo.
Uamuzi huo umefanywa na uongozi mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ulioingia madarakani Oktoba 12, mwaka huu tofauti wa awali uliotoa msimamo kuwa timu za Simba na Yanga zina mashabiki wengi hivyo uwanja huo ni mdogo (unaingiza mashabiki wachache 7,000) hivyo kutokuwa salama.
Na Mwandishi Wetu



No comments:
Post a Comment