ANGALIZO: Kuelekea Mitihani ya Darasa la 7 kesho...NECTA imesema Itavifutia Usajili Vituo Vyote Vya Mitihaini ambavyo...#share
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), limesema litavifutia
usajili vituo vyote vya kufanyia mitihani ya Darasa la Saba kwa vituo ambavyo
wamiliki wake wataingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani inayotarajiwa kufanyika kesho na kesho kutwa
yani Septemba 6 hadi 7 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo jijini Dar es Salaam na
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde wakati akizungumza na waandishi wa
habari, amesema wamiliki wanatakiwa kujua kuwa shule zao ni vituo maalumu vya
kufanyia mitihani tu.
“Baraza linawataka wamiliki wa shule zote kutambua kuwa shule
zao ni vituo maalum vya kufanyia mitihani, hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote
kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani hiyo.
“Baraza halitasita kukifuta kituo chochote cha mitihani
endapo litabaini na kuthibitisha pasina shaka kuwa kituo hicho kinajihusisha na
udanganyifu wa mitihani.
Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa kipindi
hiki cha mitihani ili wanafunzi wafanye mitihani yao kwa utulivu.
“Tunawaasa walimu, wamiliki wa shule, wasimamizi na jamii kwa
ujumla kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote. Wataokiuka haya hatutasita
kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” amesisitiza Msonde.
Ameeleza kuwa wanafunzi hao watafanya masomo matano ambayo
ni: Kiswahili, Hisabati, Maarifa ya Jamii, Sayansi na English ambapo mitihani
hiyo imeshasafirishwa kupelekwa vituoni.
Na Abraham Ntambara



No comments:
Post a Comment