sPORTS nEWS: Kampuni ya Ubashiri ya Sokabet yaimwagia mamilioni klabu ya Majimaji....#share
KAMPUNI ya Ubashiri ya Sokabet imeipatia klabu ya Wanalizombe Majimaji ya Songea udhamini wa thamani ya sh. milioni 150 utakaodumu kwa mwaka mmoja.
Akizungumza wakati wa kutiliana saini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Sokabet nchini Franco Ruhinda, amesema lengo la kampuni hiyo ni kuleta mapinduzi makubwa katia soka nchini.
"Tanzania ni nchi inayopenda soka, hivyo kwa kulitambua hilo tumeona kama Sokabet kuanza kuleta mapinduzi katika michezo kupitia udhamini huu kwa klabu ya Majimaji wa sh. milioni 150 kwa mwaka mmoja," alisema Ruhinda.
Aidha amesema kuwa ufadhili huo ni sehemu ya kurudisha sehemu ya faida wanayopata kwa jamii inayowazunguka ili kuweza kuwanufaisha kupitia soka kwani soka limekuwa sehemu ya ajira kwa vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sokabet Shane Leahy, amesema ufadhili huo ni mwanzo tu katika kuleta maendeleo ya soka kupitia klabu hiyo na kubainisha kuwa watafanya mambo mengine makubwa zaidi.
Mwenyekiti wa Majimaji Steven Ngonyani ameshukuru kwa udhamini huo wa Sokabet na kuahidi klabu hiyo kufanya vizuri katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania Bara na kuhakikisha wanachukuwa ubingwa.
Naye Dani Mrwanda akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake ameeleza kufurahia kwa ufadhili huo na kusema kwamba wanadeni kubwa kwa viongozi na wanasongea na kuahidi kupambana na kufanya vizuri ili kuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa Majimaji.
Na Abraham Ntambara



No comments:
Post a Comment