Waziri Ummy awaonya Watumishi wa Afya watakaotoa huduma mbovu kwa Wazee....#share


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watumishi wa afya kutoa huduma bora kwa wazee na kwamba serikali haitakuwa na msamaha kwa watumishi watakaokiuka agizo hilo. 


Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi vitambulisho maalumu kwa wazee 7299 wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo waliojiandikisha kwa awamu ya kwanza ambavyo vitawasaidia katika kupata huduma za kiafya bure.

"Niwatake watumishi wa afya kutoa huduma bora za afya kwa wazee wote, hakutakuwa na msamaha kwa atakayeripotiwa kukiuka agizo hilo," alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine waziri Ummy ameahidi kuwapatia bima ya afya watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu katika wilaya hiyo huku uandikishwaji wa watoto hao ukianza leo.

Aidha ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya.Ahadi hiyo ilitolewa baada ya ombi la Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Ubungo.

Ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili kupunguza mzigo kwa halmashauri katika kulinda afya za wananchi 

Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob amebainisha kuwa kwa wazee wote wa halmashauri ya Ubungo ambao hawakujiandikisha katika awamu ya watapewa nafasi ya kujiandikisha kupitia ofisi zao za serikali za mitaa.

Amesema vitambulisho hivyo vitatumika kwenye vituo vyote vya afya vya manispaa ya ubungo na hospitali nyingine kubwa nchini kwa kufata utaratibu wa upatikanaji wa rufaa huku akihaidi kukamilika zoezi hilo septemba 30 mwaka huu.

Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search