sPORTS nEWS: Mchakato wa Bilionea MO Dewji kumilikishwa Simba hatua za mwisho kukamilika..Kamati maalumu yatangazwa leo kusimamia mchakato huo....#share
KATIKA kile ambacho tunaweza kusema kwamba ni hatua za mwisho mwisho kwa klabu ya Simba kukamilisha mchakato wa kumilikiwa kwa mfumo wa hisa. Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo leo imetangaza kamati maalumu ya kusimamia mchakato wa zabuni wa kumpata mwekezaji katika mfumo huo.
Katika mfumo huo mpya asilimia 50 ya kampuni itakayoanzishwa, itatolewa kwa mwekezaji/wawekezaji atakayetokana miongoni mwa wanachama wa Simba SC kupitia mchakato wa zabuni.
Kamati hiyo maalumu iliyotangazwa itaongozwa na Jaji Msataafu wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo kama Mwenyekiti samaba na wajumbe wanne ambao ni Mussa Azzan Zungu, Abdulrazaq Badru ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini, Wakili Damas Ndumbaro na Yusuph Maggid Nassoro.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment