Kumbilamoto awataka wakazi Ilala kujiandaa kwa mikopo...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
WAKAZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jinini Dar es
Salaam, wametakiwa kujiandaa kuchukua mikopo ya halmsahuri inayotarajiwa kuanza
kutolewa hivi karibuni ili iwasaidie kujikwamua kiuchumi.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na baadhi ya wakazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa jana jijini humo na Naibu Meya wa Halmashauri ambaye
pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto alipokuwa akizungumza na
wakazi wa kata hiyo.
“Kwa hiyo sasa tupo kwenye michakato ya kujua je itumike benki
hii ya DCB au tutoke tutumie CRDB au tutaangalia benki gani ambayo itakuwa na
faida,” amesema Kumbilamoto.
Kumbilamoto amesema fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya
wananchi ni takribani zaidi ya bilioni tano na itatolewa kwa akina mama asilimia
4, vijana asilimia 4 na asilimia 2 kwa walemavu.
Amesisitiza kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa vikundi vya
kuanzia watu watano ambapo amesema utaratibu utakapokamilika wakuanza kutolewa
kwa mikopo hiyo watawatangazia.
Akizungumzia kuhusu miundombinu ya barabara amesema, barabara
ya kwa Mnyamani ipokatika hatua za mwisho kuanza matengenezo kwani mkandarasi
amekwishapatikana na ipo chini ya usimamizi wa Tarula.
Kwa upande mwingine Naibu Meya huyo ametoa misaada ya zaidi ya.
Sh. milioni 2 kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali na timu za mpira wa
miguu.
Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo, wamempongeza Diwani huyo
kwa kuwa karibu nao kwa kuwapatia misaada hiyo na kuahidi kuendelea kushirikiana
naye kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Matukio katika picha
No comments:
Post a Comment