sPORTS nEWS: Mwamuzi Simba na Yanga kuziamua Stars Botswana Uhuru kesho ........#share

MWAMUZI wa kimataifa, Elly Sasii atachezesha mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Zebras ‘Pundamilia’ ya Botswana kesho kwenye uwanja wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.


Elly Sasii  ambaye alichezesha mchezo wa Ngao ya Jamii hivi karibuni ambao Simba iliifunga kwa mikwaju ya penalti 5-4  atasaidiwa na Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania  (TFF), mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni, kiingilio ni sh. 10,000 kwa Jukwaa Kuu na sh. 5,000 kwa mzunguko.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga leo Ijumaa amezungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Hosteli ya TFF, Karume jijini Dar es Salaam ambako amethibitisha kwamba kikosi chake kiko imara kwa mapambano.
Kocha wa Botswana, David Bright amesema ingawa hana muda mrefu kwenye timu ameteua kikosi chenye mchanganyiko wa vijana na wazoefu aliokuja nao kuwajaribu .

Wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje waliofika ni nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya),Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Simon Msuva (Difaa El Jadidah ya Morocco).

Wengine  ni makipa Aishi Manula (Simba), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Yanga).
Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Yanga), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba) na Erasto Nyoni (Simba).

Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba), Said Ndemla (Simba), Shiza Kichuya (Simba), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Yanga), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Yanga).

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search