sPORTS nEWS: Ni Bundelsliga Wiki hii Freiburg wanahitaji muujiza kushinda dhidi ya Borussia Dortmund....#sahre
Borussia Dortmund watakopoumana na Freiburg kwenye
Bundesliga, matokeo tayari yameshafahamika na wengi, kwani michezo 12 ambayo
timu hizo zimekutana maokeo yalikuwa dhahiri.
Dortmund watasafiri kuelekea dimba la Schwarzwald Stadion
mjini Freiburg wakiwa wameshinda mara 12 dhidi ya timu hiyo, huku Freiburg mara
ya mwisho wakishinda mwaka 2010.
Na kama haitoshi, Dortmund kiwango Bora kabisa na inaashiria
ushindi tayari ni halali kwao. Dortmund wako kwenye kilele cha Msimamo wa ligi
ya Bundesliga wakiwa wamejikusanyia point 6 kutoka katika michezo miwili ambayo
wameshacheza huku Freiburg wakiwa na pointi moja tu baada ya kutoka sare na Frankfurt.
Kitu kinachoweza kuwapa hamasa Freiburg ni kwamba wachezaji
wengi wa Dortmund wametoka kutumikia timu zao za Taifa hivyo watakibiliwa na
uchovu tofauti na ilivyo kwa wachezaji wa Freiburg ambao waliendelea na
mazoezi. Pia kuondoka kwa mfaransa Ousmane Dembele pengine kutawapunguzia kasi
Dortmund.
Kwa upande mwingine Maximilian Philipp ambaye amenufaika na
kuondoka kwa Dembele, msimu ulipoita alikuwa kipenzi cha Mashabiki katika dimba
la Schwarzwald Stadion. Maxi alitimkia Dortmund kwa ada ya uhamisho ya Pauni
mil. 20 na sasa amejihakikishia namba katika kikosi cha Kwanza cha Borussia
Dortmund baada ya Dembele kuondoka klabuni hapo. Maximilian Philipp sasa
anacheza pamoja na Mgabon tishio Pierre Emerick Aubameyang.
Mturuki Nuri Sahin aliyejiunga na Real Madrid mwaka 2011
akitokea Dortmund kabla ya kurejea tena akipitia Liverpool, anasema anaelewa
kwa nini Dembele ametimkia Barcelona.
“Sisi sio Barcelona na tumezungumza kwamba kama Barcelona
wanaweza kumpoteza Neymar, sisi hatuwezi
kujificha, kwenye ulimwengu wa Soka siku zote kuna hatua ya zaidi yako, sisi
pia tunanunua wachezaji kutoka klabu nyingine, hii itaendelea kuwepo”
Jumamosi hii watazamaji kote Africa wataweza kutazama LIVE
mchezo kati ya Freiburg na Borussia Dortmund utakaorushwa MUBASHARA kupitia
StarTimes ambao wana kibali Pekee cha kuonyesha matangazo hayo.




No comments:
Post a Comment