Sports News: Simba Yaweka Hadharani Taarifa za Kufukuzwa kwa OMOG....Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share



Klabu ya Simba haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mabadiliko yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasioitakia mema klabu yetu.

‘Nimeshaeleza toka awali kuwa, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumwondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo.

'Tunaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka Imani yao kwa Uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi kuwa tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo' amesema Haji 
Manara alipoongea na Simba News kuhusiana na ujumbe unaosambazwa wa kuvunjwa kwa benchi la ufundi la Simba.

Klabu ya Simba itaendelea kuhakikisha inatoa taarifa sahihi na kwa wakati kupitia njia zake za mawasiliano chini ya Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Manara na sio kwingineko

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search