Mwendokasi Waua Mmoja na Wengine Zaidi ya 60 wajeruhiwa...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share

MTU mmoja amefariki na wengine zaidi ya 60 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Allys Sports kupinduka katika barabara kuu ya Shinyanga kwenda Mkoani Mwanza.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Simon Haule amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambao ulipelekea basi hilo kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali ya hiyo.

"Majeruhi wengi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Kola ndoto iliyopo Mwadui na wengine wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa shinyanga kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Dereva wa gari hilo amekimbia mara ilipotokea ajali", amesema Kamanda Haule.

Kwa upande mwingine, Jeshi la Polisi la mkoa wa Shinyanga limesema linaendelea kumsaka dereva aliyesababisha ajali hiyo na kutoroka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search