StarTimes Yawataka Watanzania Kujitokeza Katika Msimu Wapili wa Shindano la Kusaka Vipaji Uingizaji wa Sauti..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360
KAMPUNI
ya Star Media Tanzani imewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
shindano la kusaka vipaji vya sautu ili kupata watu watakao chukuliwa kwa ajili
ya kuingiza sauti kwenye filamu, tamthilia na katika elimu.

Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari na wageni mbalimbali kwenye awamu ya kwanza ya kuandaa shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania litakalofanyika Dar Es Salaam, Mwanza na Zanzibar.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko na Mahusiano wa
StarTimes Juma Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi
wa msimu wa pili wa shindano hilo kupitia
chaneli yake ya Star Swahili .
“Tunafurahi
kuzindua msimu wa pili wa shindano la uingizaji wa sauti, hii ni nafasi ya
watanzania kuonyesha vipaji vyao kwa lugha asili ya Afrika na pia kupata ajira,”
amesema Sharobaro.
Aidha
kwa msimu huu washiriki watafanyiwa usaili katika vituo vitatu ambavyo ni
Zanzibar itakuwa Septemba 30, Mwanza Septemba 7 na Dar es Salaam Oktoba 14.
Sharobaro
amefafanua kuwa jiji la Dar es Salaam watachukua washindi kumi, Mwanza
watachukua washindi watano na Zanzibar watachukua washindi watano hao
wote wataingia fainali inayotarajiwa kuwa Oktoba 28 mwaka huu kwa kuhusisha washirikisha 20 na watachuliwa
washindi 10.
Washindi
wa Shindano la kusaka vipaji vya sauti watapata fursa ya kwenda kufanya kazi
katika makao makuu ya Startimes yaliyopo jijini Beijing nchini China.
Naye Katibu
Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi amesema
kuwa Startimes Tanzania wanasaidia kukuza vipaji vya vijana pamoja na kukuza
kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
Amewaasa
Startimes kuangalia namna ya wasanii hao kunufaika na kazi zao mara baada ya
kumaliza mikataba. Pia alisisitiza kuwepo namna ya kunufaika kati ya nchi mbili
ambazo ni Tanzania na Chini katika kazi hizo za sanaa.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dkt. Seleman Sewangi
akizungumza kwenye mkutano wa kwanza kati ya Startimes Tanzania pamoja na
waandishi wa habari unaohusu shindano la kusaka vipaji vya sauti linaloandaliwa
na kampuni ya Startimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania.
Mhadhiri
kutoka Taasisi ta Taaluma za Kiswahili(UDSM), George Mrikaria akizungumza
kuhusu chuo hicho kitavyoweza kwenda sambamba na Startimes ili kuweza
kuwapata washindi wazuri watakaoitangaza pamoja na kukitangaza kiswahili katika
nchi mbalimbali hasa nchini China.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment