Waziri Nchemba Awajibu Chadema Kuhusu Vyombo vya Nje kufanya Uchunguzi Shambulio la Lissu..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema kuwa
watu wanaofanya uhalifu dakika zao zinahesabika kwani Serikali imejipanga
kuhakikisha inalinda usalama wa Wananchi.
Kauli hiyo amekuja siku kadhaa baada ya kuibuka kwa matukio
mbalimbali ya uhalifu nchini kwa baadhi ya watu kushambuliwa kwa risasi akiwemo
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu na taarifa zikidai wahalifu hao
hawajulikani.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kinampanda wilaya ya
Iramba mkoani Singida leo waziri Nchemba
amewataka wananchi kuwa na amani kwani
anaimani kubwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini katika kulinda raia na
mali zao.
“Mimi ndiye niliyepewa dhamana ya usalama wa raia na mali zao
katika wizara ya mambo ya ndani basi hapatatokea hata kakitongoji kamoja au
kauchochoro ambacho kitaonekana kimeshindikana ndani ya nchi yetu,”amesema
Nchemba.
Waziri Nchemba ameongeza kuwa nchi hii ni nchi huru ambayo inajitegemea
na kuna watu wanasema wanataka vyombo vya nje vifanye uchunguzi, hawa watu
wanao fanya uhalifu nchini, upelelezi utafanywa na watu wetu, watakamatwa na
vyombo vyetu na watafikishwa katika vyombo vya sheria vya hapahapa
tunatakiwa kuamini vyombo vyetu, kama serikali tutashugulikano kwelikweli
na si kama hatujaanza nao tunashughulika nao.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment