TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yawakingia kifua wakazi wa Loliondo...Yazuia operesheni kuwaondoa katika makazi yao kwa nguvu...#share

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa zuio la muda kusitisha operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu wananchi katika maeneo wanayoishi na kuwachomea makazi (maboma) yao huko Loliondo Wilaya ya Ngorongoro.



Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo na Mwenyekiti wa THBUB Bahame Nyanduga, imesema lengo la zuio hilo ni  ili kulinda haki za pande zote.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tume imechukua hatua hiyo kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 130(1) (f) na (h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Kifungu cha 25(1) (d) cha Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Sura ya 391) ya Sheria za Tanzania.

Aidha hatua hiyo imefikiwa kufuatia Tume kupokea malalamiko ya wananchi walioathiriwa na zoezi hilo kutoka Tarafa ya Loliondo Wilayani Ngorongoro, ambapo imeanza kufanyia uchunguzi malalamiko hayo.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
THBUB yatoa zuio la kusitisha operesheni ya kuwahamisha na kuwachomea wananchi wa Loliondo makazi yao

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jana (Septemba 4, 2017) ilitoa zuio la muda (interim order) kusitisha operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu wananchi katika maeneo wanayoishi na kuwachomea makazi (maboma) yao huko Loliondo Wilaya ya Ngorongoro ili kulinda haki za pande zote.

Tume imechukua hatua hiyo kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 130(1) (f) na (h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Kifungu cha 25(1) (d) cha Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Sura ya 391) ya Sheria za Tanzania.

Hatua hii imefikiwa kufuatia Tume kupokea malalamiko ya wananchi walioathiriwa na zoezi hilo kutoka Tarafa ya Loliondo Wilayani Ngorongoro, ambapo imeanza kufanyia uchunguzi malalamiko hayo.

Kwa mujibu wa taarifa za wananchi hao katika operesheni hiyo iliyoanza Agosti 12, 2017 na inayotekelezwa kwa pamoja na uongozi wa Wilaya ya Ngorongoro, askari wa wanyamapori kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti (SENAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Jeshi la Polisi wilayani Ngorongoro kumekuwepo na uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Wananchi hao wanadai kuwa wameondolewa kwa nguvu katika vijiji vyao halali vinavyotambuliwa kisheria, wamechomewa makazi yao moto isivyo halali na kuchukuliwa mifugo yao.

Pamoja na zuio hilo Tume imeziandikia mamlaka husika kuzitaka ziwasilishe kwake nyaraka zote zinazoonesha uhalali wa zoezi la kuwaondoa wananchi kwa kuwachomea makazi yao na kukamata mifugo yao.
Imetolewa na:

(SIGNED)
Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Septemba 5, 2017

Na Abraham Ntambara

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search