Wabunge UKAWA ukiacha kususia wabunge 7 CUF ...Wataja sababu nyingine Kuu iliyowakimbiza Bungeni leo...#share
WABUNGE wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi [UKAWA), wametaja leo sababu ya kutoka kwao nje ya bunge wakati wa
uapishwaji wa wabunge saba wa viti maalumu wa Chama cha Wananchi CUF na kusema
wamafanya hivyo ili kupinga kutumika na serikali.
Hayo yamebainisha na Mbunge wa Jimbo la Momba Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) David Silinde, amasema kuwa Bunge hilo
limekuwa likikandamizi upinzani na pia kutofuata sheria za nchi jamboa ambalo wanaona
siyo sawa.
Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo sababu ya wao kuamua kususia zoezi la
uapishwaji wa wabunge hao wa CUF.
"Kama ambavyo leo mmetuona hatujaingia wakati wa
kuapishwa kwa baadhi ya wabunge na sababu kubwa ya kutoingia ni kwamba
tunapinga bunge kutumika na serikali kukandamiza upinzani pili kutofuata sheria
za nchi na jambo la tatu na kubwa kuliko yote ni kwamba tunawaunga mkono
wabunge wote waliondolewa na hatufurahii,”
“Kuna vitu vikubwa sisi tunekuwa tukichukizwa navyo kama
serikali ku- entetain maamuzi katika chama ambacho kipo kwenye mgogoro kwamba
unapendelea upande mmoja unaacha upande mwingine" amesema Silende.
Aidha Silinde aliendelea kudai kuwa " Hiyo ndiyo tumekuwa tukipigania siku zote hatutaki bunge kuendelea kutumika tunataka kuwa na bunge imara waone mifano kama ilivyotokea kule Kenya kama mahakama inaweza kusimama peke yake tunataka na bunge letu liendelee kusimama peke yake" amesitiza Silinde

Na Mwandishi wetu

No comments:
Post a Comment