UPDATES: Marekani nayo yajitosa 'shooting' ya Tundu Lissu na kulaani vikali #share
NCHI ya Marekani imeeleza kusikitishwa kwake na tukio la
kushambuliwa kwa risasi kwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) NA Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa nchi hiyo
nchini kupitia ukurasa wake wa Facebook leo umelaani kitendo hicho cha kutumia
nguvu.
“Tunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu,”
imesema taarifa hiyo.
Ubalozi huo umesema unaungana na Watanzania katika kumtakia
kheri Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ili
apone haraka.
Lissu jana majira ya mchana akiwa ndani ya gari nyumbani
kwake mkoani Dodoma alishambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasio julikana na
kupatiwa matibabu ya awali katika holspitali ya rufaa ya Dodoma.
Aidha saa sita usiku alisafirishwa kwa matibabu zaidi katika
Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema leo Ijumaa asubuhi kuwa,
Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini.
Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge, Ndugai
amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye
mkono.
Na Mwandishi Wetu.





No comments:
Post a Comment