Wanachama CCM Wakumbwa na Hufu Kuelekea Mkutano Mkuu wa NEC...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
KATIKA kuelekea uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), baadhi ya wanachama waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali matumbo
yamezidi kupata joto.

Hofu hiyo imezidi kushika kasi baada ya kauli ya Katibu wa
NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu, Ngemela Lubinga kueleza
kuwa kwa sasa chama kinapitia majina yote ya walioomba nafasi mbalimbali ndani
ya chama hicho.
Lubinga akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada
ya kumaliziaka kikao cha CCM na viongozi wa Kikoministi cha nchini Vietnam
amesema majina ya waombaji kwa nafasi mbalimbali yameanza kupitiwa.
Amesema majina hayo yatapitiwa kabla ya kuyapeleka katika
mkutano mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
“Kwa sasa wapo watu ambao wanapitia majina yote ya wagombea
ili kufanya mchujo kulingana na sifa kabla hatujayaingia katika mkutano mkuu
ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibunu, ndiyo maana leo umeona tumekuja hapa
wageni ambao ni wajumbe wa kamati kuu kutoka chama cha Kikomonisti nchini
Vietnam.
“Na amekuja hapa na timu mbalimbali ya utalii na hiyo ni
kutaka kudumisha urafiki wetu na wenzetu na wao wanataka kujifunza mambo
mbalimbali ya kilimo pamoja na mambo ya kimazingira bila kusahau kushirikishana
mambo ya kisiasa” amesema Lubinga.
Na Dany Tibason/ Mwanahalisi Online
No comments:
Post a Comment