Waziri Mkuu Majaliwa amewagiza watendaji wa Mikoa yote nchini kufuatilia viwanda...#share
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha
wanafuatilia maendeleo ya viwanda mbalimbali katika maeneo yao.
Amesema
mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda unalenga kuinua uchumi wa Taifa
kutoka wa chini kwenda wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) alipozungumza na
watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro alipofanya ziara katika kiwanda cha
Moproco.
Alisema
licha ya kukuza uchumi wa Taifa, viwanda vitasaidia katika kutatua tatizo la
ukosefu wa ajira hususani kwa vijana kwani vinauwezo wa kuajiri watu wengi.
“Viwanda
hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu
wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake.”
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha
wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija.
Alisema
kwa muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo
lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.
Hata
hivyo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda
mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na
uzalishaji.
Pia
aliwataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ili kuviwezesha
viwanda kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi ndani ya chini.
Awali
Meneja Mkuu wa kiwanda cha Moproco, Bw. Arif Abood aliiomba Serikali kuongeza
kodi kwa mafuta yanayotoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani.
Alisema
uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kwa kiasi kukubwa ulichangia kufungwa
kwa viwanda vya ndani vya mafuta kutokana na kukosa soko.
Katika
ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Mheshimiwa Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment