Coutinho hana furaha tena Liverpool, dili la kwenda Barcelona la mmwaga machozi...#share

KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool Philippe Coutinho ameshindwa kuzuia hisia zake na ameonekana wazi kuwa na huzuni nyingi baada ya dili lake la kuhamia Barcelona kushindikana.


Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil amemwaga machozi akiwa kwenye jukumu la kuitumikia Timu yake ya Taifa kwani alikuwa  akihusishwa kwa muda mrefu kuihama Liverpool katika dirisha la majira ya kiangazi lililofungwa.

Coutinho mwenye umri wa miaka 25 katika kuhakikisha anahamia Barcelona alipeleka ombi kushinikiza uhamisho huo ambao hata hivyo haukuwezekana baada ya klabu yake kudai ada ya uhamisho ya paundi milioni 185.

Mbrazili huyo,  ambaye alikubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitano Merseyside Januari, yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Brazili akijiandaa kwa mechi ya Jumanne kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Colombia.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, kiungo huyo alionekana mwenye huzuni alipotaarifiwa kuwa ndoto zake za kucheza Camp Nou zimekufa.

Inaaminika Barcelona walitoa ofa tano kwa ajili ya Coutinho, ya mwisho kabisa ikiwa ni ofa ya paundi milioni 113 na nyongeza nyingine.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search