Waziri Nchemba Amtaja Aliyemtishia Bastola Mbunge wa Mtama Nape..Pia Azungumza Kupotea Kwa Ben Sanane wa Chadema...Soma Habari Kamili na Matukio360...#share

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema aliyemtishia bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, hakuwa askari.


Waziri nchemba amebainisha hayo leo akizungumza na kituo cha Televisheni cha Clouds, amesema mtu huyo  alikuwa ni mhalifu aliyetumia nafasi ya mkutano wa Nape na waandishi habari kutaka kumpiga risasi lakini aliishia kumtishia bastola.

“Awali tulidhani yule kijana ni polisi lakini hakuwa na sare za polisi, cha kwanza nilimuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kufuatilia na akaleta majibu kuwa hakuwa polisi,” amesema Nchemba.

Aidha, amesema suala la aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti nwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Ben Sanane ni ngumu kulisemea kwamba amefariki au yuko kwani polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

“Kwa aina ya taarifa ninazopata ni kama inaelekea kufikia ukomo ni jambo ambalo tumelipa uzito kulifanyia kazi na Mtanzania yeyote mwenye nia njema anaweza kutusaidia kufuatilia,” amesema.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

2 comments

  1. Your heading still misleading! You need to wake up on that. Don't sensationalise the heading while the story is different

    ReplyDelete
  2. Your heading still misleading! You need to wake up on that. Don't sensationalise the heading while the story is different

    ReplyDelete

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search