ACT Wazalendo kuwasilisha hoja Bungeni dhidi ya Serikali ..soma habari kamili na Matukio360...#share

 Na Mwandishi wetu
 CHAMA cha ACT Wazalendo kinatarajia kuwasilisha hoja Bungeni ikishutumu Serikali kuchukua fedha kinyemela kwenye Mashirika ya Umma kinyume na utaratibu na sharia.


Mhe Zitto Kabwe 
Taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe imeandika  “ ACT Wazalendo kinatarajia  kuwasilisha Hoja Bungeni kwa Serikali kuchota Fedha za Mashirika ya Umma kinyume cha Sheria.”

Taarifa hiyo hajatoa maelezo kwa kina na bila kutaja majina ya mashirika hayo lakini kimsingi mwasilishaji  hoja hiyo ni Zitto mwenyewe kwa kuwa ndie mbunge pekee wa chama hicho Bungeni.


Zitto aliwahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya mahesabu ya mashirika ya umma kwa kipindi cha miaka 10.

Uenda hoja hiyo ikiwasilishwa mwaka huu au mwakani kulingana na utaratibu wa Bunge unavyoelekeza.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search