Serikali yaombwa iwekeze kwenye ngoma za asili...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
Wasanii wa ngoma ya asili ya kabila la wangoni wakitumbuiza katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya
WASANII wa ngoma za
asili Mkoani Mbeya wameiomba Serikali iwawezesha na kutangaza ngoma za asili za
makabila ya mikoa ya nyanda za juu kusini
Akizungumza na
Matukio360 jijini Mbeya Mkurugenzi wa Kikundi cha asili cha kabila la wangoni, Seif
Seif amesema ngoma za asili za makabili ya mikoa ya kusini hazitambuliki
vizuri katika mikoa mingine na nje ya
nchi.
“Nyanda za juu kuna ngoma
za asili za makabila mengi sasa Serikali kupitia kwa viongozi hususan wabunge
wawekeze katika vikundi vya mila na desturi na si kuzitumia wakati wa kampeni za uchaguzi.”
"Mfano mzuri kwa
Naibu Spika Tulia Ackson aliandaa mashindano ya kushindanisha ngoma za asili wilayani Rungwe na hiyo ni njema kwa
wazawa na
kujitengenezea upendo mkubwa kwa wanarungwe."amesema.
Seif amesema njia
pekee ni kuboresha utamaduni wa mtanzania mahala popote, makabila yatambuliwe
na kuheshimika na kwamba itajenga na
kuboresha zaidi uzalendo nchini.
No comments:
Post a Comment