Afungwa jela maisha kwa kubaka mtoto..soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Mkazi wa Dar es Salaam Faraja Said kwenda jela maisha kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 8.
Imedaiwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo Disemba mwaka 2015. Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ritha Tarimo akitoa hukumu hiyo amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa ambapo ilikuta mshtakiwa ana kesi ya kujibu.
Katika ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye ndio mtoto aliyebakwa alieleza namna mshtakiwa huyo alivyombaka na kuonesha kuwa kweli mshtakiwa alifanya kosa hilo.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Daktari wa hospitali ya Amana alithibitisha mtoto huyo alibakwa ambapo alipomchukua vipimo waligundu ameingiliwa kumwili na kukuta michubuko.
Hakimu alimuuliza mshtakiwa kama ana chochote cha kuiambia Mahakama kabla ya kutoa adhabu ambapo alijibu anaomba apunguziwe adhabau ana Mke na watoto wanamtegemea.
Mwendesha mashtaka Anuciantha Leopold amesema hakuna kumbukumbu za makosa ya nyuma ya mshtakiwa hivyo apawe adhabu ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama yake. Hakimu alimuhukumu kwenda jela maisha.
No comments:
Post a Comment