Zitto, Nassari wamjibu msemaji mkuu wa Serikali...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi wetu
SIKU chahe baada ya Serikali
kulichkulia hatua za kisheria gazeti la Tanzania Daima ikidai inaendeleza
kuandika habari za uongo, mbunge Zitto Kabwe na Joshua Nassari wamejibu mapigo
kwa nyakati tofauti kuhusu sakata hilo.
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe
Jana msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi
mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abass alitangaza kulifungia kwa siku
90 gazeti la Tanzania Daima.
Leo kwa nyakati tofauti
mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amemjibu Dk Abass kuwa naye asubiri kupewa
tuzo kutokana na kufungia ovyo magazeti.
‘Unafurahia sana kufunga magazeti.
Na wewe upewe nishani ya kufungia magazeti mengi zaidi katika muda mfupi tangu
Uhuru 1961.’ Ameandika Zitto ambaye pia ni kiongozi mkuu wa chama cha
ACT-Wazalendo katika ukurasa wake wa Tweeter
Naye mbunge wa Arumeru
Mashariki Joshua Nassari katika ukarasa wake wa Tweeter ameandika ‘ Ni sahihi
barua za @Msigwa Gerson kuwa ni typing errors ila wengine ni kosa la
kuchukuliwa hatua.’
Kwa kipindi cha miaka miwili
tayari serikali imeshafungia magazeti manne ambayo ni Mseto, Mwanahalisi, Raia
Mwema na Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment