Mbunge Ester Bulaya Chadema, Adai Watu Wasiojulikana Kuhatarisha Maisha yake..Soma Habari Kamili na Sikiliza Sauti Akithibitisha Hilo na Matukio360..#share
MBUNGE wa Jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Ester Bulaya, amesema maisha yake yapo hatarini kutokana na kufuatiliwa na watu ambao anahisi sio wazuri huku wakiwa wamevalia mavazi ya ninja, nyumbani kwake wilayani Bunda.

Kauli hiyo amietoa wakati akizungumza na mwandishi wa kituo kimoja cha televisheni hapa nchini, amesema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa na gari ya Noah huku wamevalia kinija, bahati nzuri hakuwepo nyumbani hivyo ndugu zake wakamwambia asirudi nyumbani siku hiyo.
Aidha Bulaya amefafanua kwamba watu hao walizunguka kwa baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.
Msikilize Hapa Akibainisha Taarifa Hiyo
No comments:
Post a Comment