Chadema wamvaa IGP Simon Sirro..Soma habari kamili na Matukio360..#share

CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ( IGP),  Simon  Sirro kuacha kutoa vitisho kwa wananchi na wanasiasa kwa kuwataka waache kuzungumzia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  (Tundu Lissu kupigwa risasi 38 mkoani Dodoma kwa kuwa hiyo siyo kazi yake.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro

Chadema wamesema hakuna sheria yoyote inayompa Sirro mamlaka hayo na kwamba anatakiwa kuacha kutoa kauli za kuwanyamazisha.

Kauli hiyo ya Chadema, imetolewa leo na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya  alipozungumza na chombo kimoja cha habari makao makuu ya chama hicho.
Amesema Sirro hana ubavu wa kuzuia watu wakiwamo wanasiasa kuendelea kujadili suala hilo.
“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki na fursa kwa wananchi kutoa maoni na mawazo yao na kupashana habari pamoja na sheria nyingine na  ibara hii ndio msingi, ” amesema Malya.
Aidha,  ameeleza kuwa Sirro anaongozwa na sheria kubwa ya jeshi la polisi na huduma saidizi ambayo inatoa maelezo ya nani anaweza kumuamuru, na kuwa na mamlaka ya kuamuru askari wake na siyo  raia wa kawaida.
“IGP anyamaze andelee na upelelezi, msisikilize Sirro anachoeleza hamvunji sheria kwa kujadili nani amejaribu kumuua Tundu Lissu, msiingilie upelelezi wao sawa, msiwazuie kufanya upelelezi  sawa lakini jadilini,” amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search