Waziri Jafo asema hatahamisha watumishi...Soma habari kamili na Matukio360...#share
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Said Jafo amesema hatahamisha Mkuu wa Idara wala Kitengo katika Wizara yake lakini atamtengeneza awe kama anavyotaka ili aweze kuendana na kasi ya utendakaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hii ambapo aliambatana na Manaibu Waziri wa OR-TAMISEMI .
Waziri Jaffo alisema kuwa “Siwezi kuhamisha matatizo kutoka eneo kwenda lingine cha msingi ni kuhakikisha tunamtengeneza hapa hapa awe kama tunavyotaka kulingana na mahitaji yetu na aweze kuendana na kasi ya Serikali hii sasa hivi kasi yetu sio ya kutembea bali ni kukimbia na lazima wote twenda pamoja”.
Watumishi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia kikao na Waziri pamoja na Naibu Mawaziri (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAMISEMI –mjini Dodoma.
Katika picha ya pamoja ni viongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI (katikati) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jafo kushoto akifuatiwa na Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Sinkamba Kandege (Afya,Miundombinu, ViwandanaUwekezaji, naSerikalizaMitaa), KatibuMkuu OR TAMISEMIMhandisiMusa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Zainab Chaula na kulia n iNaibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. George Joseph Kakunda (Elimu, Maji, Kilimo, MifugonaMaliasili), NaibuKatibuMkuu –ElimuTixonNzunda(Elimu) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu Tanzania (TSC) Winfrida G.Rutaindurwa.



No comments:
Post a Comment