CUF Kushirikiana na Ukawa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani ..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimetangaza kushiriki uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata 43 hapa nchini unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
CUF kimesema katika uchaguzi huo kitashirikiana na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ili kuunganisha nguvu za kisiasa.
Ukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa ambavyo ni CUF, Chadema , NCCR-Mageuzi , na NRD.
Uchaguzi huo ni matokeo unafanyika kutokana na sababu zikiwamo wa vifo vya madiwani, kujiuzuru ama kuhama vyama na hivyo nafasi zao kubaki wazi.
CUF kimeweka mkakati wa kushiriki uchaguzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Ukawa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Mbalala Maharagande, ambapo ameleeza kuwa Chama hicho kimepanga kutoa tamko rasimi juu makubaliano ya Ukawa juu uchaguzi huo Tarehe 8 hadi 11 Oktoba mwaka huu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Oktoba 4 mwaka huu ilitangaza kufanyika uchaguzi huo mdogo katika kata mbalimbali chini.
NFaki Sosi

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search