Hatimaye Bilionea Manji Yupo Huru..Ni Baada ya Kuibwaga Serikali ya JPM Kwa Mara Nyingine leo..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

MFANYABIASHARA Maarufu nchini  na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Yusuf Manji ameachiwa huru leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia  upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake yailiyokuwa yakimkabili ya matumizi ya dawa za kulevya . 
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa shtaka lake.

Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.




Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa hukumu na kujulikana kuwa upande wa mashtaka hawakuweza kuthibitisha kama kweli alikuwa anatumia dawa za kulevya.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akielekea kwenye gari kwaajili ya kuondoka huku akiwa hana kosa mara baada ya kusomewa hukumu  na kuonekana kuwa hakuwa akitumia dawa za kulevya.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akipanda gari akipanda gari mara baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabiri ya kutumia dawa za kulevya ikiwa upande wa mastaka walishindwa kuthibitisha shtaka hilo.

Wakili wa Manji Bi. Hajra Mungula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya mteja wake kuonekana hana kosa la matumizi ya dawa za kulevya.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search