Dk. Kweka: Wanawake jitokezeni kupima Saratani mapema...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
WANAWAKE nchini wametakiwa kuwa
na mwamko wa kwenda hospitali kila mwaka kufanyiwa uchunguzi wa Magonjwa ya
Saratani hususani ya Shingo ya Kizazi kwani unapogundulika katika hatua za
mapema unatibika.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya TMJ, Dk.Walter Kweka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya
TMJ, Dk.Walter Kweka wakati akizunzungumza na waandishi wa habari wakati wa
zoezi la utoaji elimu na upimaji wa ugonjwa huo kwa walimu jijini hapa.
Zoezi hilo limeratibiwa na
Hospitali ya TMJ kwa kushirikianiana na Lion Klabu ya Dar es Salaam.
“Watu watengeneze ule mwamko wa
kwenda kuchunguza afya zao Kwa mfano unapozungumzia saratani ya matiti mtu
yeyote ambaye anaona mabadiliko katika matiti, kwa mwananume na kwa mwanamke
kwa sababu imezoeleka labda saratani ni ya akina mama tu ya matiti, na kwa
wanaume pia inawakuta,”
“Kwa hiyo unapoona kuna tabia
yoyote ya tofauti ndani ya kifua au matiti watu wawe na mwamko kwenda kuchunguza,
tunapozungumzia saratani ya shingo ya kizazi wakina mama wawe na tabia
yakufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi kila mwaka kwa sababu tunapugundua
tatizo mapema tunaweza kuwasaidia mapema.
Akizungumzia kuhusu elimu wanayo
toa kwa walimu hao, Dk. Kweka amesema elimu hiyo itawaongezea ufahamu katika
masuala ya saratani, ikiwemo ya shingo ya kizazi pamoja na saratani ya matiti
na saratani nyingine.
Amesema lengo ni kwamba wanapojua
waweze kujisaidia pamoja na kusaidia katika kuibua wagonjwa ambao wanakuwa na
dalili za ugonjwa huo mapema katika jamii ili waweze kufika sehemu sahihi kwa
ajili ya kufanya uchunguzi mapema kwani unapogundulika ukiwa kwenye hatua za
awali unatibika.
Ameongeza kuwa wamechoka kupokea
wagonjwa ambao wemekwishachelewa na mwisho wa siku mzigo kuwa kwa hospitali na
madaktari kwa kushindwa kumsaidia.
Gavana wa Lion Klabu kwa nchi za Tanzania, Uganda na Sudani Kusini Rizwan Qudri akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kwa upende wake Gavana wa Lion
Klabu kwa nchi za Tanzania, Uganda na Sudani Kusini Rizwan Qudri, amesema zoezi
hilo linafanyika bure na ni zuri kwa ajili ya walimu hao kuangalia afya zao dhidi ya ugonjwa wa
saratani ya shingo ya kizazi.
Amesema katika upimaji wa leo lengo
ni kupima walimu 100 na kuele kuwa wanatarajia pia kufanya zoezi hilo katika
maeneo mengine nchini.
Aidha amewataka watu wawe
wanajitokeza kwa wingi inapotokea fursa kama hiyo ili waweze kuchunguza afya
zao.
Baadhi ya walimu wa jijini Dar es Salaam waliojitokeza katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na kupetiwa elimu juu ya ugonjwa huo.
Baadhi ya walimu wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya kupima Saratani ya Shingo ya Kizazi wakifuatilia kwa makini elimu juu ya ugonjwa huo ikitolewa na Dk. Walter Kweka (hayupo pichani.
No comments:
Post a Comment